2 Timothy 1

1 aPaulo mtume wa Al-Masihi Isa kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu, kulingana na ile ahadi ya uzima uliomo ndani ya Al-Masihi Isa.

2 bKwa Timotheo, mwanangu mpendwa:

Neema, rehema na amani itokayo kwa Mungu Baba, na kwa Al-Masihi Isa Bwana wetu.

Shukrani Na Kutiwa Moyo

3 cNinamshukuru Mungu, ninayemtumikia kwa dhamiri safi, kama walivyofanya baba zangu, ninapokukumbuka usiku na mchana katika maombi yangu. 4 dNikiyakumbuka machozi yako, ninatamani sana kukuona ili nipate kujawa na furaha. 5 eNimekuwa nikiikumbuka imani yako ya kweli, waliokuwa nayo bibi yako Loisi na mama yako Eunike na ambayo mimi ninasadiki sasa wewe pia unayo. 6 fKwa sababu hii nakukumbusha uchochee ile karama ya Mungu, iliyowekwa ndani yako nilipokuwekea mikono yangu. 7 gMaana Mungu hakutupa roho ya woga, bali roho ya nguvu, ya upendo na ya moyo wa kiasi.

8 hKwa hiyo usione haya kushuhudia kuhusu Bwana wetu, wala usinionee haya mimi niliye mfungwa kwa ajili yake. Bali uishiriki pamoja nami taabu ya Injili, kwa kadiri ya nguvu ya Mungu, 9 iambaye alituokoa na kutuita katika mwito mtakatifu: si kwa kadiri ya matendo yetu mema bali kwa sababu ya kusudi lake mwenyewe na neema yake. Neema hii tulipewa katika Al-Masihi Isa tangu milele. 10 jLakini sasa imefunuliwa kwa kudhihirishwa kwake Mwokozi wetu, Al-Masihi Isa, ambaye amebatilisha mauti na kuleta uzima na kutokufa kwa njia ya Injili. 11 kNami nimewekwa kuwa mhubiri, mtume na mwalimu wa Injili hii. 12 lHii ndiyo sababu ninateseka namna hii, lakini sioni haya kwa maana ninamjua yeye niliyemwamini, na kusadiki ya kuwa anaweza kukilinda kile nilichokiweka amana kwake hadi siku ile.

13 mShika kwa uthabiti kielelezo cha mafundisho yenye uzima yale uliyoyasikia kwangu, pamoja na imani na upendo katika Al-Masihi Isa. 14 nIlinde ile amana uliyokabidhiwa kwa Roho Mtakatifu akaaye ndani yetu.

15 oUnajua ya kuwa watu wote katika Asia wameniacha, miongoni mwao wamo Filego na Hermogene.

16 pBwana akawahurumie watu wa nyumbani mwa Onesiforo, kwa sababu aliniburudisha mara kwa mara wala hakuionea aibu minyororo yangu. 17Badala yake, alipokuwa Rumi, alinitafuta kwa bidii mpaka akanipata. 18 qBwana na amjalie kupata rehema zake siku ile! Nawe unajua vyema jinsi alivyonisaidia huko Efeso.
Copyright information for SwhKC